Thursday, May 2, 2013

Wosia wa jay dee kama akifa kabla ya Ruge au Joe Kusaga

Lady jay dee
Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.

Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.

Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.

Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.

Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.

Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.
Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.

Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.

Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.

Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame
Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.

Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai
Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.

Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.

Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..

Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.

Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani??
Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??

Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.

Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma??
Roho gani hiyo??

Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu.Soure Jamii forum

Wednesday, May 1, 2013

Ajali mbaya yatokea Chalinze

Taarifa mpaka sasa zilizotufikia ajali mbaya imetokea mjim wa pwani Chalinze na Mpaka sasa hakuna taarifa kwa kuwepo yoyoyte aliyepoteza Maisha ila wapo waliojeruhiwa lakini mpaka sasa wana uzalendo wanafatilia ili kupata Taarifa zaidi kujua hali ya Majeruhi na kuona Wanaendeleaje

SENETA MUTULA KILONZO WA KENYA AFARIKI DUNIA

Seneta Mutula kilonzo
Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia ambae ameongea na Capital FM Nairobi, Mutula amekutwa akiwa amefariki dunia nyumbani kwake Machakos, hakuwa anaugua…
Marehemu Mutula kilonzo                                 

Chadema yamtuhumu Kinana kuhusika na biashara ya pembe za ndovu

Abdulrahman Kinana 
Dodoma. Kambi ya Upinzani Bungeni imetoa tuhuma nzito kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ikidai kuwa anajihusisha na mtandao wa ujangili nchini.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi amejibu tuhuma hiyo akisema ni za uongo huku akiituhumu kambi hiyo kuwa imedanganya wakati inajua ukweli kuhusu tuhuma dhidi ya Kinana.
Akiwasilisha maoni ya upinzani kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2013/14, Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu Maliasili, Mchungaji Peter Msigwa alisema vitendo vya ujangili vimekuwa vikilitia doa taifa kwenye jumuiya za kimataifa.
“Kwa bahati mbaya ni kwamba wahusika wengi ambao wanatajwa kwa ushahidi ni makada maarufu na wengine ni viongozi waandamizi wa CCM,” alisema Mchungaji Msigwa.
“Tumeshuhudia watuhumiwa wengine wa ujangili ambao Ikulu imediriki kuwapatia nafasi kubwa za uongozi wa taifa hili, licha ya kutajwa kwenye ripoti ya uchunguzi kuhusiana na ujangili.”
Alisema mwaka 2009, meli ya Kampuni ya Wakala wa Meli ya Sharaf Shipping inayomilikiwa na Kinana ilikamatwa China ikiwa na makontena yenye nyara za Serikali ikiyasafirisha kwenda Hong Kong.
“Nyaraka zilizopo Ofisi za Wakala wa Usajili wa Kampuni na Biashara (Brela), zinaonyesha kuwa kampuni hiyo ya Kinana ilisajiliwa Oktoba 2003 na kupewa hati na. 47221.
“Nyaraka zinaonyesha kuwa Kinana anamiliki hisa 7,500 kati ya 10,000 za kampuni hiyo iliyosajiliwa Dar es Salaam. Mshirika mwenzake katika kampuni hiyo, Rahma Hussein ambaye ni mke wake anamiliki hisa 2,500,” alisema Msigwa.

Dk Nchimbi ajibu mapigo
Akijibu tuhuma hizo, Waziri Nchimbi alisema: “Ukiona mtu anasimama na kuamua kusema kuwa hakuna kinachofanywa na wizara kuhusu masuala ya ujangili, ni wazi uelewa wake unakuwa na utata mkubwa.”
Alisema hoja zilizojengwa dhidi ya Kinana ni uongo mtupu... “Nimejaribu kufuatilia kwa makini alichokisema alikimaanisha, alikielewa, alikitafakari au aliandikiwa tu akaenda kusoma? Baada ya kutafakari kwa kina nikagundua hakuwa na nia mbaya, aliandikiwa tu na ameenda kusoma,” alisema Dk Nchimbi.
Alisema ukweli wa jambo hilo ni kwamba ipo tofauti ya majukumu ya kampuni za Wakala wa Meli na shughuli za kupakia mizigo bandarini huku akituhumu kambi ya upinzani kuwa inajua ukweli lakini imeamua kupotosha umma.
Dk Nchimbi ambaye alikuwa mchangiaji wa kwanza, alisema wakala hawezi kuwa mmiliki wa meli, bali anamwakilisha mwenye meli kwenye shughuli ndogondogo zinazofanyika inapofika nchi fulani kama kuhudumia watumishi wa meli, mahitaji muhimu na kufanya usafi.
“Lakini kuna watu wanaitwa ‘clearing and forwarding (Kupakua na kupeleka mizigo). Napenda kukwambia Mchungaji Msigwa kuwa kazi yao ni kupeleka na kutoa mizigo bandarini,” alisema Dk Nchimbi na kuongeza;
“Kule ndiko kuna utaratibu wa upekuzi, katika utaratibu wa upekuzi mtu wa ‘shipping agency’ (wakala wa meli) hahusiki, sina shaka hata kidogo Mchungaji Msigwa analijua hili ninalolisema, ila amelifumbia macho kwa makusudi kwa masilahi yasiyokubalika katika taifa.”
Alisema kumekuwa na uvumi ambao umekuwa ukifanywa kwa makusudi kuwa Kinana anahusika na meli iliyohusika kusafirisha pembe zile.
“Uvumi huu ni uzushi, meli iliyobeba mizigo ile inaitwa Delmas Nakadha, mmiliki wake anaitwa Bus Herman Ledley jambo hili Kambi ya Upinzani Bungeni inalijua, ila kwa masilahi yasiyokubalika katika taifa wameamua kupotosha Bunge lako,” alisema.
Alisema baada ya uchunguzi wa kutosha, wahusika walibainika na ikafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi namba 3 na 4 ya mwaka 2009 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
“Hawa (anawataja) ndiyo waliopelekwa kortini, uchunguzi ulijidhihirisha kuwa ndiyo watuhumiwa wa jambo hili, Kambi ya Upinzani Bungeni inalijua,” alisema:SOURCE MWANANCHI
Abdulrahman Kinana

Tuesday, April 30, 2013

KAZI KWAKO


Je Madrid watafanikiwa kupita leo wakiwa nyumbani?

 Koccha wa Real Madrid Jose Mourinho

Team ya Madrid leo watashuka dimbani huku wakiwa na deni la magoli matatu bila ili kujiwezesha kuvuka na kutinga fainali..ila wakilishi hao wa spain watakuwa na kazi ngumu ya kutafuta namna ya kuwabana MARIO GOTZE na ILKAY GUNDOGAN.

Mbali na madrid kuanzisha miamba yake leo kipind cha mwanzo CR7,ANGEL DIMARIA akifuatiwa  GONZALO HIGUAN bdo real madrid watakuwa na kazi ngumu ya kushinda na kufanikiwa wapinzani wao wasiweze kufunga ambalo ni jambo gumu kama kuwazuia kina REUS na ROBERT LEWANDOWSKI.

Jambo ambalo Mourinho leo atakuwa analipa kipaumbile zaidi ni mashambulizi ili kuhakikisha wanapata ushindi wa zaidi ya magoli matatu tena bila kufungwa na kwa mabeki wa real madrid ni jambo gumu na wala si jepesi kuwazuia Dortimund kuondoka bila kupata goli moja ili hali kila jambo linawezekana katika mpira
Mshamuliaji wa Borrusia Dortimund R.Lewandowski
Mashabiki wengi leo wa real madrid watakuwa wanamuhofia huyu jamaa japokuwa watakuwa wanamkaribisha santiago Bernabeu mechi iliyopita alifunga magoli manne peke yake moja likipatikana kwa njia ya penatu
real madrid wakiwa mazoezini kujiandaa na mechi
Real Madrid Borussia Dortmund
Won, 3-2 vs. Manchester City (H) Won, 1-0 vs. Ajax (H)
Won, 4-1 vs. Ajax (A) Draw, 1-1 vs. Manchester City (A)
Loss, 2-1 vs. Borussia Dortmund (A) Won, 2-1 vs. Real Madrid (H)
Draw, 2-2 vs. Borussia Dortmund (H) Draw, 2-2 vs. Real Madrid (A)
Draw, 1-1 vs. Manchester City (A) Won, 4-1 vs. Ajax (A)
Won, 4-1 vs. Ajax (H) Won, 1-0 vs. Manchester City (H)
Draw, 1-1 vs. Manchester United (H) Draw, 2-2 vs. Shakhtar Donetsk (A)
Won, 2-1 vs. Manchester United (A) Won, 3-0 vs. Shakhtar Donetsk (H)
Won, 3-0 vs. Galatasaray (H) Draw, 0-0 vs. Malaga (A)
Loss, 3-2 vs. Galatasaray (A) Won, 3-2 vs. Malaga (H)
Loss, 4-1 vs. Borussia Dortmund (A) Won, 4-1 vs. Real Madrid (H)
kama madrid leo watashinda itakuwa furaha sana katika jiji la madrid na furaha kubwa kwa C.Ronaldo ukiangalia dunia nzima itakuwa inatima leo atafanya nini kuisaidia team yake na kuinusuru kutoka kwenye michuano hiyo
C.Ronalo