Saturday, April 27, 2013

UJUMBE MFUPI AMBAO MH. JOSHUA NASSARI AMEMTUMIA MKUU WA MKOA WA ARUSHA LEO KUHUSIANA NA MATUMIZI YAKE MABAYA YA MADARAKA KUMGANDAMIZA MH LEMA

Mhe. RC Salaam. Ninasikishwa sana na mambo yanayoendelea mkoani kwangu Arusha. Lakini pia nasikitika kwamba na wewe umeamua kuwa sehemu ya uonevu dhidi ya utu na haki. Hatuwezi kuvumilia movement yeyote, ya awaye yeyote yule dhidi ya kweli na usawa. " We will stand for justice, anytime, anywhere at any cost. Video zinaonyesha jinsi ambavyo lema alisaidia kutuliza jazba za wanafunzi wa uhasibu, jinsi alivyowaasa bila woga kuhusu life style yao na umuhimu wa discpline katika maisha! Kama kiongozi mwenye dhamana ya ulinzi na usalama wa mkoa ulipaswa ku-appreciate. Kinachoendelea ni yale niliyowahi kukushauri kama sio kukuonya juu ya juhudi kubwa za viongozi wa ccm na ofisi yako kutu-undermine wabunge wa chadema arusha hususani mimi na mhe. lema na ukaahidi kubadilika. Tuliaminiwa na maelfu ya watu wakatuchagua, hatupo tayari kusaliti imani hii. Najua kuna hofu kubwa kwa sababu ya chaguzi zijazo za madiwani arusha. Nipo dodoma lakini nalazimika kuja ofisini kwako jumatatu, kukushauri tena kwa mara nyingine. Kama mnaweza kumfanyia hivi mbunge, itakuwaje kwa machinga wa ngarenaro au mama ntilie wa usa river?? Nikutakie siku njema. Joshua Nassari (MB) April 27, 2013. Dodoma Joshua Nassari, Member of Parliament and Shadow Minister for Communication, Science&Technology Tanzania.

No comments: