''Lengo letu kuu katika kuimarisha biashara na uwekezaji utakuwa
ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla,'' Rais
Kenyatta alinukuliwa akisema alipokutana na Katibu Mkuu wa EAC, Dk
Richard Sezibera aliyekwenda kumtembelea ofisini kwake mjini Nairobi
Juzi.
Aliongeza kuwa kuondolewa kwa vikwazo vya biashara kupewe
kipaumbele kadiri mtangamano wa EAC unavyozidi kuimarika na kupanuka,
Shirikia Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA) limeripoti.
''Kuondolewa kwa vikwazo vya kazi na kusafiri kwa raia ndani ya
nchi wanachama kutasaidia zaidi kukua kwa biashara na kubadilishana
mawazo,'' alisema Rais Kenyatta.
''Tunaweza kufanya vizuri zaidi tukiwa katika kanda kuliko nchi mojamoja,'' aliongeza Rais.
Naye Katibu Mkuu wa EAC, Dk Sezibera alimpongza Rais kwa kushinda
uchaguzi wa rais hivi karibuni na kuwashukuru pia wananchi wa Kenya kwa
kuwa mfano wa kuigwa kwa jinsi walivyoendesha uchaguzi huo.
Dk Sezibera pia alimpatia Rais huyo maelezo mafupi kuhusu kikao
maalum kijacho cha wakuu wa nchi za EAC kitakachofanyika, Arusha,
Tanzania, Aprili 28, mwaka huu, ambacho kitakuwa cha kwanza kwake
kushiriki kama Rais wa Kenya.
No comments:
Post a Comment